Kiongozi wa wanajeshi waliofanya mapinduzi Guinea kuapishwa kuwa rais wa mpito
2021-10-01 10:03:08| cri

Kiongozi wa wanajeshi waliofanya mapinduzi nchini Guinea Kanali Mamady Doumbouya, anatarajiwa kuapishwa kuwa rais wa mpito wa nchi hiyo katika mji mkuu Conakry.

Kwa mujibu wa katiba ya mpito iliyotangazwa na jeshi lililofanya mapinduzi, katika kipindi cha mpito Kanali Mamady Doumbouya ataunda serikali ya mpito itakayoongozwa na waziri mkuu na kamati ya mpito ya taifa (CNT) yenye watu 81.