Iran haitatoa ahadi iliyozidi makubaliano ya nyuklia ya liyofikiwa
2021-10-01 08:32:18| cri

Iran haitatoa ahadi iliyozidi makubaliano ya nyuklia ya liyofikiwa_fororder_伊朗外交部发言人Saeed Khatibzadeh

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya Iran Bw. Saeed Khatibzad amesema, Iran haitakubali kutoa ahadi zaidi kuliko zile ilizotoa kwenye Makubaliano ya Nyuklia ya yaliyofikiwa kati yake na nchi nyingine, na haitalegeza msimamo wake katika suala la kuondoa vikwazo dhidi ya nchi hiyo.

Bw. Khatibzad amesema, serikali mpya ya nchi hiyo inafikiria jinsi ya kuanzisha tena mazungumzo ya suala la nyuklia, lakini inahitaji kutathmini tena mazungumzo ya awali ya Vienna.

Pia amesema, Marekani ilijiondoa katika makubaliano hayo na kuiwekea Iran vikwazo vya upande mmoja, ambavyo vimedhuru watu wa Iran na kuisababishia nchi hiyo hasara ya kiuchumi ya mabilioni ya dola za kimarekani.