Rais wa Palestina na mawaziri wa Israel wajadili mchakato wa amani
2021-10-04 09:45:52| cri

Shirika rasmi la habari la Palestina WAFA limeripoti kuwa rais wa Palestina Mahmoud Abbas amefanya mazungumzo na mawaziri wawili wa Israel kujadili mchakato wa amani kati ya pande hizo mbili katika mji wa Ramallah uliopo Ukingo wa Magharibi.

Kwenye mkutano wake na Waziri wa Afya wa Israel Nitzan Horowitz na Waziri wa Ushirikiano wa Kikanda Issawi Frej, rais Abbas amesema kuwa ni muhimu kumaliza uvamizi wa Israel na kufikia amani kamili katika eneo hilo, kupitia utekelezaji wa maazimio ya kimataifa.

Mawaziri hao wawili wa Israel walimuelezea rais Abbas msimamo wao, ambao ni kuunga mkono ufumbuzi wa nchi hizo mbili na ushirikiano wa pamoja ili kujenga imani kati ya pande hizo mbili.