Madhara ya Ukeketaji kwa Wasichana na Wanawake
2021-10-05 07:56:11| Cri

Madhara ya Ukeketaji kwa Wasichana na Wanawake_fororder_非洲女童

Ukeketaji ni mila ambayo inapingwa vikali sana lakini bado inaendelea kufuatwa na baadhi ya makabila. Watoto wa kike wakiwa ndio waathirika namba moja wanapofanyiwa vitendo hivi baadhi yao hupoteza maisha kutokana na kuvuja damu nyingi baada ya kufanyiwa ukeketaji. Kuna baadhi ya wanawake pia wanashikilia mila hii na kutaka iendelee. Na hii inatokana na kwamba wao wenyewe walikeketwa na pia wengi wao waliolewa wakiwa na umri mdogo sana. Kwa hiyo wanaona mila hiyo ni nzuri na inampa mwanamke hadhi katika jamii. Je kweli tunaweza kuitokomeza mila hii potovu na ambayo imeshapitwa na wakati? Katika Ukumbi wa Wanawake leo hii tutaangalia madhila yanayokumba mtoto wa kike na wanawake kwa ujumla kuhusu mila hii ya ukeketaji.