CMG yasema itaendelea kuwakaribisha wasanii kutoka Taiwan kushiriki kwenye vipindi vyake
2021-10-05 15:03:16| cri

Shirika kuu la Utangazaji la China CMG limesema litaendelea kuwakaribisha wasanii kutoka Taiwan kushiriki kwenye vipindi vyake.

CMG imeyasema hayo kufuatia wasanii kutoka Taiwan kushambuliwa na kutishiwa na vyombo vya habari kisiwani Taiwan vinavyokitaka kisiwa hicho kijitenge na China bara baada ya wao kushiriki kwenye kipindi maalumu cha kusherehekea siku ya taifa la Jamhuri ya Watu wa China kilichoandaliwa na CMG.