Balozi wa China kwenye UM asema demokrasia ya kweli haipaswi kutafsiriwa na nchi chache
2021-10-05 10:27:58| CRI

Balozi wa China kwenye UM asema demokrasia ya kweli haipaswi kutafsiriwa na nchi chache_fororder_33

Mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva, balozi Chen Xu amesema hakuna kielelezo maalumu cha demokrasia, na demokrasia ya kweli haipaswi kutafsiriwa na nchi chache tu.

Akitoa taarifa ya pamoja kwenye kikao cha 48 cha Baraza la Haki za Binadamu, kwa niaba ya kundi la nchi kadhaa juu ya mada ya demokrasia na haki za binadamu, balozi Chen amesema amani, maendeleo, usawa, haki, demokrasia na uhuru vinawakilisha thamani ya pamoja ya binadamu.

Amesisitiza kuwa cha muhimu katika demokrasia ya kweli ni kuona kama inafaa kwenye hali fulani ya nchi, kama inawakilisha matakwa ya watu, kulinda maslahi ya watu na kufurahia uungaji mkono wake, na kama inaleta utulivu wa kisiasa, maendeleo ya jamii na maisha bora kwa watu. Balozi Chen pia amebainisha kuwa wana wasiwasi na vigezo viwili au hata vitatu vinavyotumika kwenye demokrasia, ambapo demokrasia inatumika kama nyenzo ya kuweka thamani ya mtu na kielelezo cha kisiasa na nyinginezo.