China yaihimiza Marekani kuacha kuunga mkono nguvu za ufarakanishaji wa Taiwan
2021-10-05 10:25:59| CRI

China yaihimiza Marekani kuacha kuunga mkono nguvu za ufarakanishaji wa Taiwan_fororder_11

Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying jana alisema Marekani inapaswa kuacha kuunga mkono nguvu za ufarakanishaji zinazotaka “Taiwan ijitenge na China”, na kuchukua hatua madhubuti katika kudumisha amani na utulivu wa Mlangobahari wa Taiwan.

Hua alisema hayo wakati alipojibu swali juu ya taarifa husika iliyotolewa na msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya Marekani Bw. Ned Price. Hua amesema Taiwan ni sehemu ya China, Marekani haina haki ya kutoa kauli zisizowajibika. Kauli husika za Marekani zinakiuka vikali kanuni za kuwepo kwa China moja na taarifa tatu za pamoja za China na Marekani, na zinatoa ishara isiyo sahihi hata kidogo na isiyowajibika.

Ameongeza kuwa China itachukua hatua zote za lazima na kuvunja kithabiti njama yoyote ya “ufarakanishaji wa Taiwan”. China ina dhamira imara katika kulinda mamlaka ya taifa na ukamilifu wa ardhi. Marekani inapaswa kusahihisha makosa yake, na kuacha kuziunga mkono nguvu za ufarakanishaji wa Taiwan.