Xi Jinping ampongeza Fumio Kishida kwa kuwa waziri mkuu wa Japan
2021-10-05 10:24:45| CRI

Rais Xi Jinping wa China jana alimtumia salamu za pongezi Fumio Kishida kwa kuchaguliwa kuwa waziri mkuu wa Japan.

Xi amesema kuendeleza uhusiano wa ujirani mwema na ushirikiano kati ya China na Japan kunaendana na maslahi makuu ya wananchi wa nchi hizo mbili, pia kutasaidia amani, utulivu na ustawi wa Asia na dunia. Ameongeza kuwa China na Japan zinapaswa kufuata kanuni zilizowekwa kwenye nyaraka nne za kisiasa kati ya nchi mbili, kuimarisha mawasiliano, kuongeza uaminifu na ushirikiano, na kufanya juhudi za kujenga uhusiano kati ya China na Japan unaolingana na mahitaji ya zama mpya.

Wakati huohuo, waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang pia amempongeza mwenzake wa Japan Kishida. Li amesema pande zote mbili zinapaswa kudumisha makubaliano ya kisiasa, kuimarisha mawasiliano na ushirikiano, kuhimiza uhusiano wa nchi mbili uendelee kwa utulivu na kuelekea njia sahihi, na kukaribisha kwa pamoja Maadhimisho ya miaka 50 tangu uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Japan urejee kwenye hali ya kawaida ambayo yatafanyika mwakani.