AMISOM yawapiga msasa wanajeshi wake ili kupiga jeki operesheni za kulinda amani katika Afrika
2021-10-06 09:40:26| CRI

AMISOM yawapiga msasa wanajeshi wake ili kupiga jeki operesheni za kulinda amani katika Afrika_fororder_33

Tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) imesema maafisa wake waandamizi wameanza mafunzo ya siku tano ili kupiga jeki operesheni zao za kusaidia amani katika Afrika.

Tume hiyo imesema inashirikiana na Kituo cha Kimataifa cha Mafunzo ya Kulinda Amani cha Kofi Annan kutoa mafunzo kwa maafisa waandamizi juu ya ufuatiliaji na tathmini kwenye operesheni za kusaidia amani. Simon Mulongo, naibu mkuu wa tume ya AMISOM amesema mafunzo hayo yameandaliwa kwenye muktadha wa Afrika na changamoto wanazokumbana nazo walinda amani ili kuhakikisha bara hilo linakuwa salama na tulivu. Mulongo ametilia mkazo kwamba kama tume ni muhimu kujifunza taratibu bora ili kuhakikisha AMISOM inafanya kazi kwa ufanisi kwenye majumu yake.