Watoto wa Kenya wahisi athari mbaya ya janga la COVID-19 dhidi ya afya ya akili
2021-10-06 09:43:55| CRI

Watoto wa Kenya wahisi athari mbaya ya janga la COVID-19 dhidi ya afya ya akili_fororder_22

Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limesema watoto wa Kenya walikuwa katika hatari kubwa zaidi ya kukabiliwa na vitendo vya ukatili na pia kukosa masomo wakati shule zinafungwa kufuatia janga la COVID-19.

Mwakilishi wa UNICEF nchini Kenya Maniza Zaman amesema shirika hilo la Umoja wa Mataifa limetuma ujumbe kwa walimu zaidi ya laki tatu wa Kenya kuhusu jinsi ya kushughulikia athari mbaya ya COVID-19 kwa wanafunzi hao.

Akiongea kwenye utoaji wa ripoti ya UNICEF kuhusu watoto duniani ya mwaka 2021 mjini Nairobi, Zaman amesema kuwa kama watoto wa sehemu nyingine, watoto na vijana wa Kenya pia wamehisi athari mbaya ya janga la COVID-19 dhidi ya afya yao ya kiakili.

Amekumbusha kuwa UNICEF ilifanya kazi kuhakikisha kuwa watoto wanapata msaada wanaohitaji ikiwemo kutumia laini ya simu kwa ajili ya kutoa msaada.