IMF yasema ukuaji wa uchumi duniani utakuwa wa “wastani kidogo” mwaka huu kufuatia kuongezeka kwa hatari
2021-10-06 09:41:36| CRI

IMF yasema ukuaji wa uchumi duniani utakuwa wa “wastani kidogo” mwaka huu kufuatia kuongezeka kwa hatari_fororder_11

Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) sasa unatarajia ukuaji wa uchumi duniani utakuwa wa “wastani kidogo” mwaka huu kwani hatari za uwiano wa ufufukaji wa uchumi duniani zimekuwa zikionekana wazi. 

Akihutubia kwa njia ya video kufuatia mikutano ya mwaka ya IMF na Benki ya Dunia iliyopangwa kufanyika wiki ijayo, Mkurugenzi Mtendaji wa IMF Kristalina Georgieva amesema dunia inakabiliwa na ufufukaji wa uchumi ambao unasuasua kutokana na janga la Corona na athari zake, na kushindwa kusonga mbele vizuri. Amebainisha kuwa kizuizi kikubwa kilichopo ni “Pengo Kubwa la Mgawanyo wa Chanjo” ambapo nchi nyingi zinapata chanjo kidogo sana, na kusababisha watu wengi kukosa kulindwa dhidi ya virusi vya Corona.

Aidha amesema wakati Marekani na China zinabaki kuwa injini muhimu za ukuaji duniani, kwenye nchi nyingine nyingi, ukuaji unaendelea kusuasua, ukizuliwa na upatikanaji mdogo wa chanjo na vikwazo vya sera.