Marais wa Misri na Palestina wajadili mchakato wa amani wa Palestina na Israel
2021-10-07 10:05:03| CRI

Rais Abdel-Fattah al-Sisi wa Misri amefanya mazungumzo na Rais Mahmoud Abbas wa Palestina kwa njia ya simu na kujadili mchakato wa amani kati ya Palestina na Israel.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya rais ya Misri imesema kuwa viongozi hao wawili wamepitia upya maendeleo ya hivi karibuni ya hatua ya Wapalestina na mchakato wa amani.

Rais Sisi alisisitiza juhudi za nchi yake ikishirikiana na Wapalestina katika kufufua mchakato wa amani kwa ajili ya kuwarejeshea haki watu wa Palestina na kuhimiza usalama na utulivu katika eneo hilo.

Abbas alipongeza uhusiano wa Wamisri na Wapalestina, akisema kuwa Palestina inathamini juhudi na hatua ya Misri katika kusukuma mbele kazi ya Palestina na kufikia suluhisho la haki na la kina.

Aidha marais hao wawili walikubaliana kuendeleza mazungumzo na ushirikiano wa pande mbili katika kipindi kijacho kuhusu maswala ya maslahi ya pamoja.