Walinzi wa amani wa UM watumwa Matchika, CAR baada ya shambulizi lililosababisha vifo
2021-10-07 09:58:59| CRI

Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric jana alisema walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa wametumwa wilayani Matchika nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), ili kukusanya habari zaidi juu ya shambulizi lililosababisha vifo na kuhakikisha kuwalinda raia.

Amesema idadi ya vifo na majeruhi ya raia bado haijajulikana. Tume ya kulinda amani imetoa wito kwa serikali kufanya uchunguzi, ili wahalifu watambuliwe na kuwafikisha mbele ya sheria. Tume hiyo pia imelaani vikali shambulizi hilo lililotokea Jumanne wilayani Matchika, kilomita takriban 15 kutoka Bambari, mji mkuu wa Jimbo la Ouaka, katikati mwa CAR.