Marekani yatakiwa kuchukua hatua halisi kutekeleza matokeo ya mazungumzo ya simu kati ya viongozi wa nchi yake na China
2021-10-08 09:55:58| CRI

Marekani yatakiwa kuchukua hatua halisi kutekeleza matokeo ya mazungumzo ya simu kati ya viongozi wa nchi yake na China_fororder_11

Mkurugenzi wa ofisi ya kamisheni ya mambo ya nje ya kamati kuu ya CPC Yang Jiechi amekutana na mshauri wa masuala ya usalama wa kitaifa wa rais wa Marekani Jake Sullivan huko Zurich, Uswizi, ambapo pande mbili zimekubaliana kuchukua hatua ili kutekeleza matokeo ya mazungumzo ya simu kati ya viongozi wa nchi zao, kufanya juhudi za kuhimiza uhusiano kati ya nchi hizo mbili uelekee kwenye njia sahihi yenye maendeleo tulivu.

Katika miaka ya hivi karibuni, uhusiano kati ya China na Marekani umeporomoka sana. Sababu ni kuwa Marekani imefanya makosa makubwa ya kimkakati dhidi ya China, na kuelewa vibaya uhusiano kati ya pande hizo mbili. Kwa hivyo, kuimarisha mawasiliano ya kimkakati kati ya pande hizo mbili, haswa kurekebisha maoni potofu juu ya China, kuna umuhimu mkubwa katika kuhimiza uhusiano kati ya pande mbili urudi kwenye hali ya kawaida.

Kwanza Marekani inapaswa kuelewa kwa kina hali ya kunufaishana na kusaidiana kwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili. Kuna taarifa za upotoshaji nchini Marekani ambapo inaaminika kuwa China imekuwa ikijipatia faida kutoka Marekani. Lakini ukweli ni kuwa thamani ya jumla ya biashara kati ya China na Marekani imeongezeka kutoka chini ya dola za kimarekani bilioni 2.5 ya mwaka 1979, hadi kufikia dola za kimarekani bilioni 629.5 ya mwaka 2020. Ripoti iliyotolewa hivi karibuni na Chama cha Wafanyabiashara cha China na Marekani imeonesha kuwa, imani ya makampuni ya Marekani juu ya China imerejea katika kiwango kilichokuwa kabla ya kukumbwa na janga la Corona, na kufikia kiwango cha juu zaidi katika miaka mitatu iliyopita.

Wakati huo huo, Marekani inapaswa kutambua kwa usahihi sera za ndani na za kigeni za China na nia ya kimkakati. China imesisitiza mara kwa mara kuwa, haina nia ya kuchochea au kuchukua nafasi ya Marekani, bali inataka kujiongeza bila kusita. China haina mkakati wa kutafuta umwamba, ila tu ina mkakati wa kujiendeleza ambao lengo lake ni kuwafanya wananchi waishi maisha mazuri. Baadhi ya Wamarekani wanaichukulia China kama “mshindani mkubwa wa kimkakati” au hata “adui wa kufikirika”, na kuhamisha majukumu yake ya masuala ya ndani kwa China. Changamoto kubwa inayoikabili Marekani siku zote inatoka ndani ya Marekani yenyewe, kwa hivyo ni bora ijitahidi kushughulikia vizuri mambo yake na kuifanya kuwa nchi bora zaidi.