Jukwaa la kidijitali la Umoja wa Afrika lazinduliwa ili kuhimiza ujumuishaji wa fedha
2021-10-08 09:53:18| CRI

Jukwaa la kidijitali la Umoja wa Afrika lilizinduliwa jana Alhamis jijini Nairobi nchini Kenya ili kuhimiza ujumuishaji wa fedha barani Afrika ambako takriban watu milioni 400 wanatengwa kwenye mfumo rasmi wa fedha.

Likizinduliwa na AfricaNenda, muungano unaojitegemea wa wataalamu wa malipo ya kidijitali, ni jukwaa ambalo linatafuta kuunganisha teknolojia zinazoibukia ili kurahisisha miamala kufuatia kufufuka hatua kwa hatua kwa biashara ya kuvuka mpaka.

Maureen Mbaka, katibu mkuuu wa Wizara ya TEHAMA, Uvumbuzi na Masuala ya Vijana amesema uzinduzi huo wa jukwaa la malipo ya kidijitali utachochea ukuaji wa uchumi unaotegemea maarifa katika Afrika mbali na kurahisisha ujumuishaji wa fedha kwa wale waliotengwa.