Algeria yadai “heshima kamili” kutoka Ufaransa ili kumrejesha balozi wake huko Paris
2021-10-11 09:05:51| CRI

Rais Abdelmadjid Tebboune wa Algeria amethibitisha kuwa kumrejesha balozi wa nchi hiyo huko Paris kutawezekana baada ya Ufaransa kutoa “heshima kamili” kwa Algeria.

Rais Tebboune amesema nchi yake haiwezi kujifanya kama hakuna jambo lililotokea, na balozi wake atarudi Paris walau baada ya Ufaransa kuonesha heshima kamili kwa Algeria.

Kauli ya rais huyo inahusiana na kumrudisha balozi wake kutoka Ufaransa na kupiga marufuku ndege za jeshi la Ufaransa kuingia katika anga ya nchi hiyo, kufuatia taarifa iliyotolewa na rais Emmanuel Macron wa Ufaransa wiki iliyopita ikiukosoa utawala wa Algeria.