Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC zapoteza asilimia 92 ya pato la utalii kutokana na janga la Corona
2021-10-11 09:04:33| CRI

Nchi 6 wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC zimepoteza asilimia 92 ya mapato yanayotokana na sekta ya utalii kutokana na janga la COVID-19.

Katibu mkuu wa jumuiya hiyo Bw. Peter Mathuki ametoa taarifa ikisema, idadi ya watalii waliowasili katika kanda hiyo imepungua kutoka milioni 6.98 kabla ya janga hadi milioni 2.25 ya hivi sasa, ikisababisha hasara kubwa ya kiuchumi.

Amesema kanda hiyo imefunguliwa tena kwa ajili ya biashara, huku akihimiza serikali za nchi wanachama na wadau wengine kufanya juhudi kwa pamoja kutangaza vivutio vya utalii vya kanda hiyo, ili kuhakikisha ufufukaji wa kasi wa sekta hiyo.