Semina ya uzinduzi wa Chaneli ya Olimpiki ya CMG yafanyika Beijing
2021-10-11 20:42:13| Cri

Semina ya wataalamu kuhusu uzinduzi wa Chaneli ya Olimpiki ya Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG imefanyika leo hapa Beijing.

Naibu mkuu wa Idara ya Uenezi ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC na mkuu wa CMG Bw. Shen Haixiong amesema kwenye semina hiyo kuwa uzinduzi wa Chaneli hiyo ni hatua muhimu ya kukuza michezo ya Olimpiki nchini China, na jukumu la kwanza ni kuhudumia Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing na Michezo ya Olimpiki ya Watu wenye Ulemavu, kuandaa mazingira mazuri ya kufanyika kwa Michezo hiyo miongoni mwa watu wa China, na pia kuwahamasisha watu milioni 300 kushiriki kwenye michezo ya baridi, na kuonesha tamasha kubwa na la kuvutia la michezo ya baridi kwa watazamaji duniani.