Wajasiriamali wa China ni kati ya washindi kwenye mashindano ya uvumbuzi ya kundi la nchi 20
2021-10-11 08:50:54| CRI

Kampuni ya Sansure Biotech ya China imepata tuzo ya uvumbuzi kwenye sekta ya afya kwenye mashindano ya uvumbuzi ya kundi la nchi 20 (G20) yaliyoshindanisha makampuni 100 kutoka nchi 20.

Mashindano hayo yaliyofanyika moja kwa moja na kwa njia ya mtandao wa internet katika mji wa Sorrento kusini mwa Italia, yalikuwa na sehemu tano, kila sehemu ikilenga changamoto zinazowakabili binadamu, kwenye mambo ya usafi, akili bandia, muunganiko wa vitu na vifaa vya kuvaa, miji yenye teknolojia za kisasa na afya.

Kampuni ya Sansure Biotech ya China inatengeneza vitendanishi na vifaa vya kisasa vya upimaji vinavyotumika katika kupima maambukizi ya COVID-19. Kampuni hiyo pia imeonyesha bidhaa mpya zinazoweza kupima virusi kwa kasi zaidi na kwa ufanisi mkubwa zaidi.