Mkuu wa UM atoa wito wa kuingiza ukwasi kwenye uchumi wa Afghanistan
2021-10-12 09:10:07| CRI

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres jana Jumatatu alitoa wito wa kuingiza ukwasi kwenye uchumi wa Afghanistan ili kuufanya uchumi huo uwe na uhai.

Bw. Guterres amesema mbali na msaada wa kibinadamu, jumuiya ya kimataifa inahitaji kuchukua hatua kuzuia uchumi wa Afghanistan usiporomoke. Ameonya kuwa bila chukula, ajira, na bila haki zao kulindwa, watu wengi zaidi wa Afghanistan watakimbia makazi yao na kutafuta maisha bora. Wakati huohuo, magendo ya dawa za kulevya, mitandao ya uhalifu na ugaidi pia vinaweza kuongezeka, hali ambayo si kama tu itaiathiri vibaya Afghanistan yenyewe, na bali pia itaathiri kanda nzima na hata dunia nzima.

Katibu mkuu huyo amesema suala la kuingiza ukwasi linapaswa kutendewa kwa njia tofauti na masuala mengine, kama vile suala la utambuzi wa serikali ya Afghanistan, suala la vikwazo na kuzuia mali.