Rais wa China ahutubia mkutano wa kilele wa COP15
2021-10-12 15:18:07| CRI

Rais Xi Jinping wa China leo amehudhuria na kuhutubia mkutano wa kilele wa Kikao cha 15 wa Pande zilizosaini Mkataba wa Anuwai ya Viumbe (COP 15) kwa njia ya mtandao.

Kwenye hotuba yake, Rais Xi amesema mazingira ya kiikolojia si kama tu ni mali ya asili, bali pia ni mali ya kiuchumi, na yanahusisha uwezo wa maendeleo ya uchumi na jamii, hivyo inapaswa kuanzisha njia ya kuendeleza uchumi usiochafua mazingira. Amesema janga la COVID-19 limeleta changamoto zaidi kwa Ajenda ya Mwaka 2030 ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa, hivyo inapaswa kuwa na mshikamano zaidi, na kuyafanya matokeo ya maendeleo na mazingira mazuri ya kiikolojia yanufaishe watu wa nchi mbalimbali kwa haki.

Rais Xi amesema, China imepiga hatua dhahiri katika juhudi za kuboresha mazingira ya kiikolojia, na itaendelea kusukuma mbele juhudi hizo, kwa kufuata mawazo mapya ya maendeleo ya uvumbuzi, uratibu, kutochafua mazingira, kufungua mlango na kunufaishana.