Viongozi wa Russia, Ujerumani na Ufaransa wajadili suala la Ukraine kwa njia ya simu
2021-10-12 09:27:23| cri

Ikulu ya Russia Kremlin imesema Rais Vladimir Putin wa Russia, Chansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wamejadili suala la Ukraine kwa njia ya simu.

Taarifa iliyotolewa na Kremlin imesema kuwa hali ya mkwamo katika juhudi za kumaliza mgogoro wa Ukraine imejadiliwa kwa undani katika mazungumzo hayo. Viongozi hao watatu wote wamebainisha kuwa kufuata na kutekeleza Makubaliano ya Minsk ya mwaka 2015, ni sharti la msingi linaloweza kutatua suala hilo, huku wakitaka washauri na mawaziri wa serikali zao kujenga mawasiliano na kufanya kazi chini ya mfumo wa muundo wa Normandy.

Licha ya hayo, masuala mengine ya kimataifa yakiwemo kuhimiza juhudi za kupambana na ugaidi barani Afrika, pia yalijadiliwa kwenye mazungumzo hayo.