Rais wa Marekani kukutana na rais wa Kenya alhamisi kwenye ikulu ya Marekani
2021-10-13 09:38:14| CRI

Msemaji wa Ikulu ya Marekani Bibi Jean Psaki jana amesema rais Joe Biden wa Marekani atakutana rais Uhuru Kenyatta wa Kenya katika Ikulu ya Marekani Alhamisi.

Bibi Psaki amesema viongozi hao watajadili uhusiano kati ya pande hizo mbili na haja ya kuleta uwazi na uwajibikaji kwa mifumo ya kifedha ya ndani na kimataifa. Pia watajadili juhudi za kulinda demokrasia na haki za binadamu, kuhimiza amani na usalama, kuharakisha ukuaji wa uchumi, na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.