Watu watano wauawa katika shambulizi la kujitoa muhanga Somalia
2021-10-13 08:53:31| CRI

Watu wasiopungua watano wameuawa na wengine sita walijeruhiwa katika mlipuko wa kujitoa muhanga uliotokea jioni ya jana Jumanne katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Polisi nchini humo wamesema tukio hilo limetokea baada ya mshambuliaji wa kujitoa muhanga kujilipua ndani ya mgahawa mmoja karibu na njia panda ya Fagah, na mpaka sasa majeruhi wote wamefikishwa katika hospitali.