UM wapongeza ahadi mpya ya makubaliano ya amani ya Mali
2021-10-13 09:29:17| CRI

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric, amesema umoja huo umepongeza ahadi mpya zilizotolewa na pande za Mali kuhusu utekelezaji wa makubaliano ya amani na mpango wa serikali wa kuwarejesha wapiganaji katika jamii.

Msemaji huyo amesema Umoja wa mataifa unapongeza ahadi mpya zilizotolewa na pande mbalimbali za Mali katika kutekeleza  makubaliano ya amani, baada ya mkutano wa kamati ya usimamizi wa makubaliano kufanyika huko Bamako.

Amesema wadau wa Umoja wa Mataifa wanaipongeza serikali ya Mali kutangaza kuwarejesha kwenye jamii wapiganaji 13,000 wa zamani kabla ya mwishoni mwa mwaka huu na wengine 13,000 katika miaka miwili au mitatu ijayo, ikiwa sehemu ya mpango wa kimataifa wa kunyang’anya silaha na kuwarejesha wapiganaji kwenye jamii nchini Mali.