Waziri wa mambo ya nje ya China ahudhuria mkutano maalum wa kilele wa G20 juu ya suala la Afghanistan
2021-10-13 09:45:10| CRI

Waziri wa mambo ya nje ya China ahudhuria mkutano maalum wa kilele wa G20 juu ya suala la Afghanistan_fororder_VCG111352979700

Mjumbe Maalum wa Rais wa China na waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi, jana ameshiriki kwenye mkutano maalumu wa kilele wa Kundi la Nchi 20 (G20) juu ya suala la Afghanistan kwa njia ya video.

Bw. Wang Yi amesema uzoefu wa Afghanistan katika miaka 20 iliyopita umeonyesha kuwa kuheshimu haki ya kila nchi ya kuchagua njia yake ya maendeleo yenyewe, kuvumiliana na kufundishana kati ya ustaarabu tofauti ni njia sahihi ya kuendeleza mahusiano ya kimataifa, na sio kupandikiza itikadi kwa wengine au kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine.

Amelitaka kundi la G20 litoe mchango katika kuhimiza utulivu na ustawi wa Afghanistan, huku akitoa mapendekezo manne, ambayo ni kutanguliza maslahi ya watu wakati wa kuisaidia Afghanistan kukabiliana na msukosuko wa kibinadamu, kuzingatia hali ya sasa na pia kuangalia siku za baadaye wakati wa kuhimiza maendeleo shirikishi nchini Afghanistan, kuhakikisha nchi hiyo inaondokana na ugaidi, na kuhimiza ushirikiano kati ya mifumo mbalimbali juu ya suala la Afghanistan.