COP15 wapitisha Azimio la Kunming
2021-10-14 08:48:23| CRI

Mkutano wa ngazi ya juu wa Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Bioanuwai wa mwaka 2020 wapata matokeo matatu_fororder_7016331724401590284

Mkutano wa 15 wa Pande zilizosaini Mkataba wa Viumbe Anuwai (COP15) unaofanyika mjini Kunming, mkoa wa Yunnan, kusini magharibi mwa China umepitisha Azimio la Kunming.

Waziri wa Ikolojia na Mazingira wa China, Huang Runqiu ametangaza kupitishwa kwa Azimio hilo katika Kikao cha Ngazi ya Juu cha sehemu ya kwanza ya Mkutano huo. Amesema Azimio hilo litatoa ishara ya nguvu, kuionyesha dunia dhamira halisi ya kutafuta suluhisho la matatizo ya kupotea kwa viumbe anuai, na hatua kali zaidi kuhusu masuala yaliyojadiliwa katika kikao hicho.
Azimio la Kunming ni azimio la kisiasa na mafanikio makubwa ya mkutano huo. Azimio hilo linajikita kwenye kuhakikisha maendeleo, kupanga na kutekeleza kifanisi mpango wa dunia wa viumbe anuwai baada ya mwaka 2020, ili kubadili hali ya sasa ya upotevu wa viumbe hai na kuhakikisha kuwa anuai ya viumbe inawekwa kwenye njia ya ufufukaji itakapofika mwaka 2030, ili kutimiza kihalisi lengo la mwaka 2050 la “Kuishi kwa Masikilizano na Asili.”

Naibu waziri wa mazingira wa China Bw. Zhao Yingmin, amesema mkutano wa ngazi ya juu wa Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Bioanuwai kwa mwaka 2020 umekamilisha majukumu yake na kupata matokeo matatu muhimu.

Akiongea kwenye mkutano na wanahabari, Bw. Zhao Yingmin ametaja matokeo hayo, ambayo kwanza ni kutoa msukumo wa kisiasa wa ngazi ya juu kwa usimamizi wa bioanuwai duniani, pili ni kutoa Azimio la Kunming, na tatu ni kutangaza hatua mpya za China za kuhifadhi bioanuwai.

Ofisa huyo amesema huo ni mkutano maalumu uliofanyika wakati dunia bado inakabiliwa na changamoto kubwa za janga la Corona. Mkutano huo umekamilisha majukumu yake, kuinua dhamira ya kisiasa ya dunia katika kuhifadhi bioanuwai, na kukusanya nguvu za kimataifa kwa ajili ya usimamizi wa bioanuwai duniani.