Rais wa Zanzibar amwalika mshindi wa tuzo ya Nobel Abdulrazak Gurnah kutembelea maskani yake
2021-10-14 09:19:49| CRI

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Mwinyi amemwalika mshindi wa tuzo ya Nobel ya fasihi Abdulrazak Gurnah kutembelea Zanzibar, huku akisema ushindi wake umekifanya kisiwa hicho kujivunia.

Rais Mwinyi amesema hayo akifanya mazungumzo na mwandishi huyo wa riwaya aliyezaliwa huko Zanzibar, akiongeza kuwa ushindi wake ni fahari ya wazanzibar, watanzania na waafrika.

Bw. Gurnah mwenye umri wa miaka 73 alikulia huko Zanzibar, na mwaka 1968 alihamia Uingereza akiwa mwanafunzi. Amechapisha riwaya 10 na riwaya kadhaa fupi.