Rais Xi Jinping atoa agizo kutaka wazee wanufaike na matunda ya maendeleo na kuishi maisha mazuri
2021-10-14 08:48:57| CRI

Rais Xi Jinping atoa agizo kutaka wazee wanufaike na matunda ya maendeleo na kuishi maisha mazuri

Wakati China inaadhimisha Sikukuu ya jadi ya Tisa Tisa yaani Sikukuu ya Wazee inayoangukia leo Alhamisi, rais Xi Jinping ametoa agizo muhimu kuhusu kazi ya utunzaji wa wazee, na kuwatakia wazee wote wa China afya njema, maisha marefu na kila la heri.

Rais Xi Jinping atoa agizo kutaka wazee wanufaike na matunda ya maendeleo na kuishi maisha mazuri

Rais Xi ameziagiza kamati za Chama na serikali katika ngazi zote zitilie maanani na kufanya vizuri kazi ya kuwahudumia wazee, kutekeleza kwa makini mkakati wa taifa wa kukabiliana na kuongezeka kwa idadi ya wazee, kuendeleza mavumbuzi ya kimfumo na kuongeza sera nafuu na fedha kwenye sekta hiyo, ili kukamilisha mfumo wa huduma za jamii kwa wazee.

Rais Xi amesisitiza kuwa idara husika zinatakiwa kuongeza nguvu katika kuendeleza na kurithisha maadili ya jadi ya kuwaheshimu na kuwatunza wazee, kutelekeza vizuri sera nafuu kwa wazee, kulinda ipasavyo haki halali za wazee, ili kuhakikisha wazee wananufaika na matunda ya maendeleo na kuishi maisha mazuri ya uzeeni.