Nchi za Afrika Mashariki kujumuisha masoko ya hisa
2021-10-15 10:16:04| CRI

Mkurugenzi mtendaji mkuu wa Soko la Hisa la Nairobi NSE Bw. Geoffrey Odundo amesema, nchi za Afrika Mashariki zinafanya juhudi kujumuisha masoko ya hisa, ili kuhimiza biashara na kutoa soko kubwa zaidi kwa wawekezaji.

Bw. Odundo amesema, Kenya, Uganda na Tanzania baadaye zitakuwa na jukwaa la kidijitali litakalounganisha masoko ya nchi hizo tatu. Amesema kwa ujumla watu wataweza kufanya biashara kuhusu aina zote za hisa nchini Kenya, Uganda na Tanzania bila ya kizuizi chochote.

Bw. Odundo pia amesema, Rwanda yenye soko la hisa pia itashirikiana na nchi hizo.