Ofisa wa afya wa Kenya asema raia milioni 7.5 wanahitaji huduma ya matunzo ya macho
2021-10-15 09:17:45| CRI

Ofisa mmoja wa Wizara ya Afya ya Kenya amesema raia wapatao milioni 7.5 wa nchi hiyo wanahitaji huduma ya matunzo ya macho.

Mkuu wa huduma za macho katika Wizara ya Afya ya Kenya Bw. Michael Gichangi, amesema mjini Nairobi kuwa ni asilimia 20 tu ya watu wenye matatizo ya macho ndio wanaweza kupata huduma zenye ubora za macho.  

Akiongea kwenye maadhimisho ya Siku ya Uoni Duniani ya mwaka huu yenye kaulimbinu ya “Penda Macho Yako”, Bw. Gichangi amesema asilimia kubwa ya matatizo ya macho yanatokana na ugonjwa wa mtoto wa jicho ulioletwa na umri, ambao unaweza kutibika. Wizara ya Afya inakadiria kuwa watu laki 2.5 nchini Kenya wana upofu wa macho.