Rais Xi Jinping atoa wito wa ushirikiano kwenye uchukuzi na maendeleo ya pamoja
2021-10-15 09:20:56| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametoa wito wa kuhimiza ushirikiano kwenye sekta ya usafirishaji duniani na kuhimiza maendeleo ya pamoja wakati dunia ikikabiliana na mabadiliko makubwa na janga la COVID-19, ambavyo vyote havijawahi kutokea katika karne iliyopita.

Akihutubia kwa njia ya video ufunguzi wa mkutano wa pili wa Umoja wa Mataifa kuhusu usafirishaji endelevu, Rais Xi ametoa wito wa kufungua ukurasa mpya wa kuunganisha miundombinu, kutokwamishwa kwa biashara na uwekezaji, na mawasiliano kati ya staarabu mbalimbali.

Mkutano huo unaofanyika kutoka Alhamisi hadi Jumamosi na kuvutia wawakilishi kutoka nchi 71, unafanya mapitio ya mafanikio yaliyopatikana kwenye ajenda ya maendeleo endelevu kuelekea mwaka 2030.

Rais Xi amesema ni kwa kuwa na uwazi, ushirikishi na muunganiko ndipo nchi mbalimabali zinaweza kuimarisha nguvu zao na kuweza kunufaishana.