Tanzania yapanga kujenga chuo cha Tehama
2021-10-15 10:23:28| CRI

Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania amesema serikali ya Tanzania inapanga kujenga chuo cha kisasa cha teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama), ili kuchochea ukuaji wa uchumi.

Rais Samia amesema hayo katika kilele cha mbio za mwenge wa Uhuru na kumbukumbu ya siku ya Nyerere kwa heshima ya mwasisi wa nchi hiyo Julius Nyerere aliyefariki Oktoba 14 mwaka 1999, huku akisema serikali iko katika hatua ya mwisho kuandaa ujenzi wa chuo hicho.

Ameongeza kuwa chuo hicho kitakachokuwa kikubwa zaidi katika eneo la mashariki na kusini mwa Afrika, kinalenga kuwafanya vijana wa nchi hiyo kuwa na uvumbuzi na kuwawezesha kuchangia ukuaji wa uchumi.

Pia amesisitiza kuwa Tehama imekuwa kiini cha mapinduzi ya nne ya kiviwanda yanayoenea kote duniani.