Bibi Peng Liyuan atoa wito wa kuhimiza afya na elimu ya kidigitali kwa wasichana na wanawake
2021-10-16 12:48:39| cri

Mke wa Rais wa China Bibi Peng Liyuan, ametoa wito wa kuhimiza elimu ya kidigitali na afya kwa wasichana na wanawake, ili kukabiliana na athari za janga la COVID-19. Bibi Peng ambaye pia ni mjumbe maalum wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa maendeleo ya elimu ya wasichana na wanawake, amesema hayo kwa njia ye video kwenye utoaji wa tuzo ya UNESCO ya 2021 kwa elimu ya wasichana na wanawake Ijumaa.

Bibi Peng amesema tangu kuanzishwa kwa tuzo hiyo mwaka 2015 kupitia ushirikiano kati ya China na UNESCO, tuzo hii imeendelea kuwa na ushawishi mzuri na kuhamasisha watu zaidi kujitolea kuhimiza elimu ya wasichana na wanawake. Pia amesifu tuzo hiyo, kwa kusema makumi ya maelfu ya wasichana na wanawake wamepata ujuzi na maarifa, na kupata uwezo na ujasiri wa kubadilisha hatma yao na kufuata ndoto zao. Bibi Peng pia amesema janga la COVID-19 limekuwa na athari mbaya sana kwa elimu ya wasichana na wanawake, na kutoa mwisho wa hatua sahihi na nzuri kuchukuliwa ili kuwapatia elimu ya haki, na elimu bora zaidi.

Amehimiza elimu ya kidigitali kwa wasichana na wanawake, kutumia kikamilifu teknolojia hii, kushiriki kwenye kutumia raslimali za hali ya juu za elimu kwa njia ya internet, kuongeza msaada wa kielimu kwa wasichana na wanawake wanaoishi kwenye maeneo maskini, na kuboresha uwezo wao wa kutumia teknolojia mpya kwa ajili ya ajira na ujasiriamali.