Msemo huu maarufu umetokana na utamaduni wa Confucious, ukielezea vipindi tofauti vya maendeleo ya mtu na kuzungumzia wajibu wa mtu, familia, jamii na taifa. Unaweza kufananisha na msemo usemao “samaki mkunje angali mbichi” mtoto ukimpa maelekezo mazuri tangu akiwa mdogo atabeba wajibu wake, familia, jamii na taifa.