Tanzania yatenga dola za kimarekani milioni 39.1 kufufua sekta ya utalii
2021-10-18 08:16:46| CRI

Tanzania yatenga dola za kimarekani milioni 39.1 kufufua sekta ya utalii wakati wa janga la COVID-19_fororder_VCG111233622704

Tanzania imetenga shilingi bilioni 90.6, sawa na dola za kimarekani milioni 39.2 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi 23 ili kufufua sekta ya utalii inayoathiriwa vibaya na janga la COVID-19.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam, Waziri wa Maliasili na Utalii nchini humo, Damas Ndumbaro amesema, fedha hizo ni sehemu ya dola za kimarekani milioni 567.25 zilizoidhinishwa Septemba na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).

Ndumbaro amesema, miradi hayo ni pamoja na kukarabati miundo mbinu, kuweka mifumo ya usalama, kununua vifaa vya kupima maambukizi ya COVID-19 kwa watalii, na kununua vifaa vya usafirishaji.