Kamanda wa Al-Shabab ajisalimisha kwa jeshi la Somalia
2021-10-18 08:48:10| cri

Afisa wa jeshi la taifa la Somalia, SNA Bw. Mohamed Nur amesema, kamanda wa kundi la Al-Shabaab, Mohamed Kulow Ali, amejisalimisha kwa jeshi la Somalia lililoko katika mji wa Wajid.

Nur amesema, kamanda hiyo alikuwa akisimamia shughuli za kundi hilo kusini mwa Somalia, amejisalimisha akiwa na bunduki aina ya AK47 pamoja na risasi.

Bw. Nur aliongeza kuwa, jeshi litapokea gaidi yeyote ambaye yuko tayari kujisalimisha kulingana na agizo la msamaha wa serikali ya nchi hiyo.