Mawaziri wa mambo ya nje wa China na Zambia wazungumza kwa njia ya simu
2021-10-19 09:47:04| CRI

Mawaziri wa mambo ya nje wa China na Zambia wazungumza kwa njia ya simu_fororder_timg (2)

Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi amesema ushirikiano kati ya China na Zambia ni imara na una mustakabali mzuri.

Wang amesema hayo kwenye mazungumzo yake na mwenzake wa Zambia Stanley Kakubo yaliyofanywa kwa njia ya simu. Amempongeza Kakubo kwa kuteuliwa kuwa waziri mpya wa mambo ya nje wa Zambia, na kusema China na Zambia zote ni nchi zinazoendelea, na zina maslahi na malengo mengi ya pamoja. Ameongeza kuwa China itaendelea kuwa mshirika thabiti wa maendeleo ya Zambia, iko tayari kuziwezesha nchi za Afrika ikiwemo Zambia zinufaike na mafanikio yake ya maendeleo, na itasaidia Afrika kuharakisha maendeleo ya viwanda na kutimiza kihalisi uhuru wa kiuchumi.

Kwa upande wake, Kakubo amesema serikali mpya ya Zambia inatilia maanani sana urafiki na China, na itaimarisha zaidi ushirikiano na China katika nyanja mbalimbali. Ameongeza kuwa Zambia pia inapenda kuongeza uratibu na ushirikiano na China katika masuala ya pande hizo mbili na ya pande nyingi.