Umoja wa Mataifa watafuta taarifa zaidi kuhusu mashambulizi ya anga huko Mekelle, Ethiopia
2021-10-19 08:29:43| CRI

Umoja wa Mataifa unajitahidi kuthibitisha ripoti za mashambulizi ya anga katika eneo la makazi ya raia la Mekelle, mji mkuu wa mkoa wa Tigray, nchini Ethiopia.

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema, katibu mkuu wa Umoja huo ameeleza wasiwasi wake kuhusu athari kwa raia wanaoishi ama kufanya kazi katika eneo la tukio, na pia kuongezeka kwa vurugu katika eneo la kaskazini mwa Ethiopia.

Amesema Katibu Mkuu huyo amerejea tena wito wake wa kusimamisha vurugu, na kuzitaka pande husika kutoa kipaumbele kwa maisha ya watu na kutoa uungaji mkono unaotakiwa kwa ajili ya usafirishaji wa misaada ya kibinadamu, ikiwemo mafuta na dawa.