Shehena ya pili ya chanjo ya COVID-19 ya China yawasili Uganda
2021-10-21 08:48:56| CRI

Shehena ya pili ya msaada wa chanjo ya COVID-19 ya China imewasili Uganda jumanne wiki hii, na Balozi wa China nchini humo Bw. Zhang Lizhong alikabidhi chanjo hizo kwa waziri wa afya ya msingi wa Uganda Bi. Margaret Muhanga katika hafla iliyofanyika kwenye Bohari ya Dawa nchini humo.

Waziri Muhanga ameishukuru China kwa kutoa shehena nyingine ya chanjo kwa Uganda. Amesema shehena ya kwanza ya chanjo ilitolewa kwa makundi yaliyopewa kipaumbele wakiwemo walimu, na shehene hiyo nyingine ya chanjo itainua kiwango cha upatikanaji wa chanjo nchini Uganda na kuongeza idadi ya watu wanaopata chanjo, ili kusaidia ufufukaji wa uchumi nchini humo.

Balozi Zhang Lizhong amesema, tarehe 18 ilikuwa ni maadhimisho ya miaka 59 tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi, na kuwasili kwa chanjo hizo kumeonyesha urafiki wa kindugu kati ya China na Uganda. Amesema tangu maambukizi ya COVID-19 kutokea, China na Uganda zimesaidiana na kuungana mkono na kushirikiana katika mapambano dhidi ya janga hili.