Watu 13 wauawa baada ya basi la jeshi kushambuliwa kwa bomu mjini Damascus, Syria
2021-10-21 08:59:00| CRI

Watu 13 wameuawa na wengine watatu kujeruhiwa katika shambulizi la mabomu dhidi ya basi la jeshi lililotokea mapema Jumatano katikati mwa mji mkuu wa Syria, Damascus.

Shirika la Habari la Syria SANA limesema, mabomu yaliyotegwa kwenye basi hilo yalilipuka wakati lilipokuwa likipita Daraja la Rais lililo katikati ya Damascus.

Serikali ya Syria imelitangaza tukio hilo kuwa ni shambulizi la kigaidi, na hadi sasa hakuna kundi lolote lililokiri kuhusika na shambulizi hilo.