Mkoa wa Tibet waonyesha demokrasia na haki za binadamu nchini China
2021-10-21 08:52:07| CRI

Waziri wa Mambo ya Nje ya China Wang Yi amesema, mkoa wa Tibet umekuwa ishara dhahiri ya maendeleo ya demokrasia na haki za binadamu nchini China, na dirisha muhimu la ushirikiano wa China na dunia.

Wang amesema hayo katika hafla maalum ya Wizara hiyo iliyoandaliwa kuuwasilisha Mkoa Unaojiendesha wa Tibe ulioko kusini magharibi mwa China kwa dunia. Hafla hiyo ilihudhuriwa na mabalozi wa nchi mbambali nchini China pamoja na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa walioko China.

Wang Yi amesema, miaka 70 iliyopita, kupitia juhudi kubwa za Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Tibet ilitimiza ukombozi wa amani. Amesema kupitia uongozi wa CPC kwa zaidi ya miaka 70, watu wa makabila yote mkoani Tibet wameshikamana na kufanya kazi kwa pamoja ili kuufanya mkoa huo kuwa mfano wa mafanikio ya maendeleo ya kasi ya China.