Umoja wa Afrika watoa mafunzo ya kupambana na ugaidi kwa askari polisi wa Somalia
2021-10-22 08:58:26| CRI

Umoja wa Afrika watoa mafunzo ya kupambana na ugaidi kwa askari polisi wa Somalia_fororder_f1907b09b6434971a811fbb8374cb3c2

Tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) imeanza mradi wa mafunzo ili kuboresha uwezo wa askari polisi wa Somalia katika kupambana na ugaidi.

Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na idara ya jeshi la polisi ya AMISOM yatawasaidia askari polisi wa Mkoa wa Kusini Magharibi kuwa na uwezo wa kuzuia vitendo vya kigaidi, kubadilishana taarifa, kutafuta na kuwaondoa washukiwa wa ugaidi.

Kaimu mratibu wa polisi wa AMISOM mjini wa Baidoa, Bisong Ejue amesema, kupambana na ugaidi na kulinda jamii bado ni kipaumbele cha jeshi hilo, na kuongeza kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa jeshi la polisi la Somalia hususan kabla na baada ya uchaguzi.