Nchi za Maziwa Makuu barani Afrika zatakiwa kuboresha uhusiano kati yao
2021-10-22 08:54:37| cri

 

 

Mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun amezitaka nchi za kanda ya Maziwa Makuu ziendeleze ushirikiano, na kuboresha zaidi uhuisiano kati yao.

Akizungumza kwenye mkutano wa ngazi ya mawaziri wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliofanyika jana kuhusu suala la Maziwa Makuu barani Afrika, Balozi Zhang amesisitiza kuwa kuzidisha hali ya kuaminiana ya kisiasa na kuimarisha uhusiano wa kiuchumi ni njia yenye ufanisi ya kuboresha hali ya kanda hiyo.

Amesema China inatoa wito kwa jamii ya kimataifa kuongeza msaada wa chanjo ya COVID-19 kwa nchi za kanda hiyo, na kuchukua hatua halisi katika kupunguza madeni na kusaidia maendeleo, ili kuzisaidia nchi za kanda hiyo kupambana na janga na kuharakisha ukarabati baada ya janga hilo.