Maofisa wa China na Afrika waamini mkutano wa FOCAC utakaofanyika mjini Dakar utaimarisha uhusiano kati ya pande hizo
2021-10-22 08:53:54| cri

Wawakilishi kutoka Ujumbe wa China kwenye Umoja wa Afrika, Tume ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, na Ujumbe wa kudumu wa kidiplomasia wa nchi za Afrika katika Umoja wa Afrika wamehudhuria semina yenye lengo la kutupia macho enzi mpya ya ushirikiano wa China na Afrika.

Washiriki hao wanaamini kuwa, mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika utakaofanyika mjini Dakar, Senegal, utaimarisha zaidi uhusiano kati ya China na Afrika.

Akizungumza kwenye semina hiyo, Mkuu wa ujumbe wa China kwenye Umoja wa Afrika, Bw. Liu Yuxi amesema, ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika na mshikamano katika kupambana na janga la COVID-19 umetoa nguvu kubwa kwa nchi za Afrika kuanza tena kazi na uzalishaji, na kufufua uchumi. Ameongeza kuwa, mkutano ujao wa FOCAC utahimiza ubora ushirikiano kati ya China na Afrika kwa kuzingatia hali mpya, mahitaji mapya na fursa mpya za ushirikiano.

Kwa upande wake, mwakilishi wa kudumu wa Senegal, katika Umoja wa Afrika Bineta Diop, amesema mkutano huo utaimarisha zaidi uhusiano kati ya China na Afrika, kuhimiza maendeleo endelevu na kuimarisha jumuiya ya China na Afrika yenye hatma ya pamoja.