Rais wa China apongeza kuzinduliwa kwa Idhaa ya Olimpiki ya CMG
2021-10-25 16:38:53| CRI

Rais Xi Jinping wa China amepongeza Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) kwa kuzindua Idhaa ya Olimpiki ya televisheni na tovuti.

Katika barua yake ya pongezi, rais Xi amesema Idhaa hiyo inapaswa kuenzi michezo ya Olimpiki na utamaduni wa michezo hiyo, kuimarisha mawasiliano na ushirikiano wa kimataifa wa michezo, na kuhimiza mawasiliano ya ustaarabu kati ya watu wa China na nchi nyingine duniani.