Rais Xi Jinping asema China kurejeshewa haki zote halali katika UM ni ushindi wa wachina na wa watu wa nchi mbalimbali duniani
2021-10-25 12:19:33| cri

Rais Xi Jinping wa China amehudhuria na kuhutubia katika mkutano wa kuadhimisha miaka 50 tangu Jamhuri ya Watu wa China irejeshewe kiti chake halali katika Umoja wa Mataifa.

Rais Xi amesisitiza kuwa katika miaka 50 iliyopita, kikao cha 26 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kilipitisha azimio nambari 2785 kwa wingi mkubwa wa kura, na kuamua kurejesha haki zote za Jamhuri ya Watu wa China katika Umoja wa Mataifa na kumtambua mjumbe wa serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kuwa mjumbe pekee halali wa China katika Umoja huo. Amesema huu ulikuwa ni ushindi wa watu wa China, na pia ni ushindi wa watu wa nchi mbalimbali duniani.

Rais Xi amesisitiza kuwa watu wa China siku zote wanashirikiana na watu wa nchi mbalimbali duniani, kulinda haki na usawa wa kimataifa, na kutoa mchango mkubwa katika amani na maendeleo ya dunia. Amesema watu wa China wanafanya juhudi kuhimiza maendeleo ya pamoja, kuanzia ujenzi wa “reli ya TAZARA” hadi “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, wametoa misaada kadri wawezavyo kwa nchi zinazoendelea, na kuendelea kutoa fursa mpya kwa dunia kutokana na maendeleo ya China.