Wang Yi akutana na kaimu naibu waziri mkuu wa serikali ya mpito ya Taliban nchini Afghanistan
2021-10-26 09:13:18| cri

Wang Yi akutana na kaimu naibu waziri mkuu wa serikali ya mpito ya Taliban nchini Afghanistan_fororder_79a23644f07649a49ff0d62d9e5d3729

Mjumbe wa Baraza la Taifa la China na Waziri wa Mambo ya Nje Wang Yi jana amekutana na naibu waziri mkuu wa serikali ya mpito ya Taliban ya Afghanistan Mullah Baradar nchini Qatar.

Wang Yi amesema kwa sasa Afghanistan iko katika kipindi muhimu cha kujikwamua kutoka kwenye ghasia na kuingia kwenyeusimamizi, na ina fursa za kihistoria za kushikilia hatma mkononi mwake, kutimiza uvumilivu na maelewano, na kujenga upya taifa. Lakini pia inakabiliawa na changamoto kuu nne zikiwemo haki za binadamu, uchumi, vita dhidi ya ugaidi na usimamizi. Amesema China inaheshimu mamlaka, uhuru na ukamilifu wa ardhi ya Afghanistan, kuunga mkono watu wa Afghanistan kuamua hatma ya taifa lao na kuchagua njia ya kujiendeleza.

Wang pia amesisitiza kuwa “Vuguvugu la Kiislamu la Mashariki ya Turkestan” ETIM ni kundi la kigaidi lililoorodheshwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, sio tu ni tishio halisi dhidi ya usalama wa taifa la China na ukamilifu wa ardhi, bali pia linatibua utulivu na usalama wa kudumu wa ndani ya Afghanistan. China imeitaka serikali ya Taliban kujitenga na makundi yote ya kigaidi ikiwemo ETIM, na kuchukua hatua halisi kupambana nayo.

Naye Baradar amefahamisha hali ya sasa ya Afghanistan na kusema itafuata njia ya maendeleo inayoendana na hali halisi ya nchi na kuchukua hatua za kuongeza ujumuishi na uwakilishi wa kisiasa wa watu ikiwemo kulinda haki za wanawake na watoto katika kupata elimu na kazi. Baradar amesisitiza kuwa serikali ya Taliban inaishukuru China kwa kuonesha urafiki katika kipindi chake kigumu. Ameahidi kuwa serikali hiyo haitaruhusu mtu yeyote au nchi yoyote kuharibu maslahi ya China kwenye ardhi ya Afghanistan.