UM waeleza wasiwasi wake juu ya kuongezeka kwa uadui kaskazini mwa Ethiopia
2021-10-26 09:11:09| cri

Umoja wa Mataifa umeeleza wasiwasi mkubwa juu ya uadui unaondelea kuongezeka kaskazini mwa Ethiopia, yakiwemo mashambulizi mapya ya anga yaliyotokea mwishoni mwa juma lililopita huko Tigray.

Ofisi ya Uratibu wa Mambo ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) Jumapili imesema, mashambulizi mawili ya anga yaliripotiwa kwenye kiwanda cha nguo katika mji wa Adwa uliopo katikati ya Tigray na mji wa May Tsebri Kaskazini magharibi mwa Tigray. Kwa mujibu wa ripoti, raia watatu walijeruhiwa huko May Tsebri.

OCHA imesema wafanyakazi wa UM walioko huko wanathibitisha taarifa zaidi za mashambulizi ya anga na matokeo yake kwa raia. Mapigano pia yameripotiwa kuendelea katika maeneo kadhaa ya mkoa jirani wa Amhara hadi kusini mwa Tigray na kwamba uadui umesababisha maelfu ya watu kukimbia makazi.