Peng Liyuan atuma salamu za pongezi kwa uzinduzi wa Kitivo cha Juilliard cha Tianjin
2021-10-27 09:17:36| cri

Peng Liyuan, mke wa rais Xi Jinping wa China, ametuma barua ya pongezi kwa uzinduzi wa Kitivo cha Juilliard cha Tianjin, ambacho kilianzishwa kwa pamoja na Chuo cha Muziki cha Tianjin na Kitivo cha Juilliard cha New York.

Kwenye barua yake Peng amesema kutokana na juhudi za pamoja kati ya China na Marekani, Chuo cha Muziki cha Tianjin na Kitivo cha Juilliard wamefanya ushirikiano wa hali ya juu wa kisanaa katika kuendesha kitivo, na kutoa jukwaa jipya la kukuza mawasiliano ya kitamaduni na kati ya watu wa nchi hizo mbili.

Pia amesisitiza kuwa sanaa ni daraja linalovuka mipaka ya nchi na kuunganisha watu, na kwamba kuimarisha ushirikiano wa elimu kati ya China na Marekani kunasaidia kukuza vipaji, kuimarisha mawasiliano ya kitamaduni, na kukuza sanaa na urafiki.

Ametoa wito kwa pande hizo mbili kufanya mabadilishano makubwa ya kitamaduni na kati ya watu, ili kukuza maelewano kati ya watu wa pande hizo mbili, na kuimarisha urafiki kati ya wachina na watu wa Marekani.